
BENDI ya extra Bongo next Level leo watatoa buruudani ndani ya Ukumbi wa Stereo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukonga nyoyo za wapenzi na mashabiki wa Sinza kwenye Ukumbi wa Meeda ikiwa na wataalamu wa kanga moja leo wanaelekea pale Kinondoni.
Akizungumza na mtandao huuu Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo , Ally Chocky aliwataka wapenzi na mashabiki wafike kujionea wenyewe mambo mapya ya Bendi yao yakiwa na mwimbaji mpya wa Bendi hiyo ,Banza Stone ambaye atatam,bulisha wimbo wake mpya wa Falsafa ya Maisha
Kiongozi wa wacheza shoo wa Bendi hiyo, Super Nyamwela aliwataka wapenzi wa Kinondoni wasisubili kusimuliwa wakaribie Kinondoni Stereo wajionee wenyewe mamabo mapya kabisa